• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
BARIADI TOWN COUNCIL
BARIADI TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri Ya Mji Bariadi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhima na Dira
    • Historia
  • Huduma
    • Leseni za Biashara
    • Hati za Viwanja
    • Tozo za Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
    • Kitengo
  • Machapisho
    • Fomu
    • Ripoti
    • Habari
    • Waraka
    • Sheria
    • Sera
    • Gazeti la Serikali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
  • Miradi
  • Tangazo
  • Michezo na Burudani
  • Zabuni

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI MJINI BARIADI

Zilizopandishwa: March 24th, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi

Dakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiasha ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.

” Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchikwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa” 

Akizungumzia gharama za ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu, Rais Magufuli ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi na Wakala wa majengo nchini TBA kukaa na kurejea gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo wa Shilingi Bilioni 46 kuwa hauendani na hali halisi ya aina ya jengo linalotakiwa kujengwa.Rais Magufuli ametoa Shilingi bilioni 10 ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo.

”Haiwezekani majengo ya ghorofa ishirini lijengwe kwa shilingi Bilioni Kumi wakati jengo la ghorofa moja moja lijengwe kwa gharama ya shilingi Bilioni 46” 

Rais Magufuli pia ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu kuendelea na ujenzi wa mradi wa tenki la maji katika mlima Ngasamo ili wananchi wa mkoa wa Simiyu ikiwemo wilaya ya Bariadi kupata huduma ya maji badala ya kukwama kutokana na mwekezaji mmoja kutaka kuchimba madini ya Nikeli katika mlima huo.

Amesema haiwezekani wananchi zaidi ya milioni moja wakose maji kutokana na mwekezaji mmoja ni kukosa muelekeo na kumkosea Mwenyezi Mungu kitu kisichokubalika hivyo Waziri wa Nishati na Madini afute leseni ya mwekezaji huyo ili wananchi wa Simiyu wapate huduma ya maji.

 Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla kutumia mvua chache zinazonyesha kulima mazao yanayostahamili ukame kama vile Mtama,viazi na Uwele ili kuweza kujikimu kwa chakula badala ya kutegemea chakula cha msaada kutoka Serikali

Matangazo

  • TANGAZO LA MRADI WA TACTIC HALMASHAURI YA MJI BARIADI March 09, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI February 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA KAZI YA UDEREVA DARAJA LA II ULIOFANYIKA TAREHE 28/02/2023 February 28, 2023
  • JINSI YA KUBADILISHA TAHUSUSI (COMBINATION) KIDATO CHA TANO June 13, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • ONGEZENI KASI KWENYE KUONYESHA MIRADI ILIYOFANYIKA

    February 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI YA MATENGENEZO YA BARABARA NA MADARAJA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 TSHS 2,060,610,000.00

    February 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI 2025/2026 BILIONI 29,235,121,948.00

    February 07, 2025
  • ONGEZENI UMAKINI NA MIKAKATI KWENYE UKUSANYAJI WA MAPATO

    February 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara ya Mhe Rais Mjini Bariadi
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Union Day
  • BARIADITC

Tovuti Mashuhuri

  • Watumishi Portal
  • OR-Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Along Bariadi-Lamadi Road

    Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi

    Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554

    Simu: ******

    Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.