KAMATI YA USALAMA MKOA YARIDHISHWA NA MIRADI YA BOOST HALMASHAURI YA MJI
Kamati ya Usalama Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.Dkt Yahaya Nawanda June 07
ilifanya ziara ya kukagua miradi na Boost katika Halmashauri ya Mji Bariadi na kusema kuwa
imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya Elimu Msingi
inayoendelea kupitia Mradi wa Boost katika Halmashauri ya hiyo na kutoa maelekezo ya kuhakikisha
kuwa miradi hiyo ikamilike na kuwa bora zaidi.
Mhe.Dkt Nawanda akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa miradi hiyo ambayo kamati hiyo
imetembelea ukiwemo mradi ya shule mpya ya nyangaka,ujenzi wa madarasa wawili ya mfano katika
shule ya msingi Bariadi,ujenzi wa shule mpya oldmaswa,ujenzi wa vyumba vitatu shule ya Msingi
ng’wang’wali A,Gamondo A,Gamondo B,Sima B pamoja na Sanungu amesema miradi inakwenda vizuri,
hivyo amewataka kuhakikisha wanaendelea na spidi hiyo ili ikamilike kwa wakati huku kipaumbele
kikiwa kwenye ubora .
Halmashauri ya Mji wa Bariadi imepokea kiasi cha shilling Billioni 1,531,200,000.00 kwa ajili ya
uboreshaji wa miundombinu ya elimu msingi kupitia mradi wa Boost.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mji Bariadi
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.