Bariaditc. Katika Kuadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha amewaongoza Wananchi Watumishi pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda kushiriki zoezi la upandaji Miti katika Shule hiyo
Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa kwa kuenzi jitihada zake za kulinda Mazingira na kukuza Maendeleo endelevu
Mhe.Macha ameungana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Simon Simalenga ,Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Imelda Kirima pamoja na wakuu wa Idara na vitengo.
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.