Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Bariadi limepitisha na kuridhia Mapendekezo ya Rasimu ya Bajeti ya Matengenezo ya barabara na Madaraja Mwaka wa Fedha 2025/2026 Tshs 2,060,610,000.00
Awali akiwasilisha rasimu hiyo ya mapendekezo ya Bajeti Kaimu Meneja wa Tarura Wilaya ya Bariadi Mhandisi Hussein Katakwebah amesema Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Bariadi (Bariadi Mji) ina jukumu la kutunza na kuendeleza barabara zenye urefu wa Kilomita 384.16 kwa mijinu wa sheria ya barabara Na .13 ya Mwaka 2007.
Aidha Mhandisi Katakwebah amesema barabara zinazohudumiwa ba Tarura Wilaya (Bariadi Mji) zina urefu wa Kilomita 384.16 kati ya barabara hizo kiomita 129.85 ni nzuri sawa na 33.8% zinaptika kwa kipindi chote cha Mwaka,Kilomita 167.68 sawa na 43.65% na kilomita 86.61 ni mbaya sawa na 22.25% ziko katika hali mbaya na zinapitika kwa shida au kuna wakati haziptiki wakati wa msimu wa mvua.
Hata hivyo Mhandisi Katakwebah amesema bajeti haitoshelezi mahitaji ukilinganisha na hali halisi ya barabara zetu na maeneo mengi kuharibiwa na mvua ila serikali imeendelea kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwa ajili ya matengenezo ya maeneo yaliyoharikibiwa na mvua huku kazi za kurekebisha zikiwa zinaendelea kadgri fedha zinavyopatikana.
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mji Bariadi
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.