Afisa Usimamizi Fedha Mwandamizi Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Charles Kilapilo amekielekeza kitengo cha Mawasiliano na Habari Serikalini kuhakikisha wanaongeza kazi ya utoaji habari ikiwemo kuchapisha kazi Za miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ili wananchi waweze kuona kazi hizo zilizofanyika kwani wao ndio wanufaika namba moja na miradi hiyo ambayo imeletewa fedha na serikali .
Aidha Kilapilo amezitaka pia taasisi Za serikali na wakuu wa idara na divisheni kuhakikisha wanahudhuria vikao vya mabaraza ya Madiwani kikamilifu na kuwasilisha taarifa mapema.
Hatahivyo Kilapilo amepongeza mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 kuwa imezingatia mambo muhimu ikiwemo ilanı ya Chama cha Mapinduzi huku akitaka kuongeza mikakati ya kuthibiti na ukusanyaji wa mapato ili Bajeti hiyo iweze kutekelezeka na kuleta manufaa kwa wananchi zaidi kwa kupeleka miradi yenye kipaumbele chao.
Kilapilo ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Bariadi cha kupitisha Mapemdekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ambayo imepitishwa na baraza hilo leo Februari 7,2025
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.