LESENI ZA BIASHARA (Business Licensing Act No 25 of 1972, Amendment 1980 and 2014)
MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu na ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai (katika kipindi cha miezi 12 iliyopita) na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na Hati ya kuishi nchini daraja `A`(Residence permit class A) na nyaraka nyingine za usajili wa kampuni yake ndio aweze kufanya biashara nchini.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi TFN 211 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Certificate of Incorporation iwapo ni kampuni na Certificate of
Registration and Extract kama ni jina la biashara.
(ii) “Memorandum and Article of Association”ambayo inaonesha kipengele ambacho kampuni hiyo inakiombea leseni ya biashara..
(iii) Passport ya Tanzania au Kitambulisho cha uraia au Kitambulisho cha mpiga kura au Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo(affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (Powers of attorney) Iwapo wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi,itolewe kwa mtanzania ambaye anaishi hapa.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
(vii) Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali, Kwa mfano (TFDA, EWURA, ERB, TPRI, TCRA, CRB, TALA, CAL) n.k lazima mwombaji kuwa na leseni husika kabla ya kuomba leseni ya biashara.
(viii) Hati za utaalam (Professional certificates) kwa biashara zote za kitaalam mfano Ushauri wa kitaalam (Consultancy), udaktari, urubani wa ndege, uhandisi nk.
Maombi mapya yanapitia ngazi zote za mwanzo kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kupitishwa au kupatiwa leseni, ambazo ni Afya, Mipango miji na Afisa biashara wa kata au eneo ambapo biashara husika inayoombewa leseni itafanyika.
MAKOSA YA LESENI ZA BIASHARA.
i. Kuendesha biashara bila leseni.
ii. Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye leseni.
iii. Kutumia leseni moja kufanyia biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi.
iv. Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyeidhinishwa na Serikali.
v. Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi.
vi. Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada/kodi inayostahili.
vii. Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.
ADHABU
Mtu yeyote anayetenda majawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs. 50,000/= na isiyozidi Tshs. 100,000 au kifungo kisichozidi
miaka miwili (2) au faini na kifungo kwa pamoja.
MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI
1. Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi.
2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.
3. Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya Biashara No. 25 ya 1972 na marekebisho yake.
4. Mwenye leseni hatatowa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na vyombo vinavyotumika kisheria.
5. Mwenye leseni anaweza kunyaganywa leseni na mamlaka iliyotoa wakati wowote ikiwa itaonekana aliipata kwa njia ya danganyifu au amekiuka msharti ya leseni.
ANGALIZO:
LESENI ZA BIASHARA HULIPIWA ADA NA KUHUISHWA (RENEW) KILA MWAKA KWA MJIBU WA SHERIA YA LESENI No. 25 YA 1972 NA MAREKEBISHO YAKE YA 2014). MFANYABIASHARA ANATAKIWA KUHUISHA LESENI YAKE YA BIASHARA NDANI YA SIKU 21 TANGU ILIPOMALIZIKA NA PENALTY YA 25% ITATOZWA KWA WANAOCHELEWA NA ITAKUWA IKIONGEZEKA KWA 2% KILA MWEZI.
VIWANGO VYA LESENI ZA BIASHARA
SIN COLUMN) COLUMN 11 COLUMNlTI COLUMN IV
BUSINESS BUSINESS CATEGORY DESCRIPTION
|
FEE FOR
PRINCIPAL LICENCE |
FEE FOR SUBSIDIARY LICENCE |
|||
Local |
300,000=
|
200,0001=
|
|||
Foreian Owned
|
3,000 USD
|
1,500 USD
|
|||
7. Medical Practitioner
|
|
|
|||
Local Foreign |
150,000/=
1,000 USD |
15o,bOOI=
1,000 usn |
|||
8.J\ny other consultancv
|
|
|
|||
Local |
200,000/=
|
100,0001=
|
|||
|
|
|
Foreign Owned
|
3,000 US!)
|
2,000 US])
|
|
|
|
9. If employees of
|
NIL |
NTL
|
|
|
|
government, Parastatal
|
|
|
|
|
|
Organization
|
|
|
|
|
|
Religious owned,
|
|
|
|
|
|
institution or Private
|
|
|
|
|
|
companies
|
|
|
10
|
General
|
Trading
|
I. Dispensary, health
|
RO,OOO/-
|
50,000/=
|
|
|
|
centre and Laboratory
|
|
|
|
|
|
Clinic
|
|
|
2. Hospital- Local
150,000/=
100,000/=
._ -
Foreign 1,000 US)) 1,000 US))
3. Selling Medicines retail
(a)parl i poison shop 200,0001- 100,0001=
-;
(blPart ii poison shop 100,000/- 80,000/=
4. Hardware and
Building materials retail
(a) City I Municipal 200,0001= 150,000/= (h) District 150,000/= 100,0001=- (c) Minor settlement and 60,000/- 50,000/=
Village -_. -
5. Workshop & Garages
(a) City / Municipal 150,0001- 100,000/= (b) District 120,0001= 100,0001= (c) Minor settlement and 100,0001- 50,000/=
Village
6. Bakeries
3U,UOO/- 30,000/=
(a) City / Municipal 100,000/= 50,000/=
SIN COLUMN I
COLUMN 11
COLUMN III
COLUMN-IY._]
BUSINESS
C.I\TEGORY
BUSINESS FEE FOR
DESCRIPTION PRINCIPAL
_ r "CENCE
FEE FOR
SU8SlI>IARY
LICENCE
--- -- - -- -1-------
. 1_1_ Auctioneers
'----
!2Q,OOOI=_
I 50,(lOO/'--
12 Seilingspar-c-pa-n-s.·-'-I-'-I-------- - --------
• JV otor Vehicle -----
(a) Cit~MLlnidpal _
_(b) I )istrict
(c) Minor settlement and
Villatic . _
300,O(Xl/-=
2S0]lOO!=
30,(KJO/=
200,COO/-'
ISO,(lO()f--
30,000/
2. M01~~)'cks
i.~_Cily !Ml~!~iIXII _ 120,()()O/ (b) DIstrict llO,O()()/-- ( c) Minor settlement - -;J-6,6oo/=
and Villa~ _
IOO,OO()/ SO,DUO!
30,(X)()/
3.Bic~ _ (a) City I MUnlcipal JQll)istrict _
( c) MinOT sct~el1len~ (d)Villagc
-- -------
·1. Industrial SparesmId
Tools
(~2Cit)' I_~~!}_i~il)ul
(b) District
(c ) Minor scttle;;';-;m
and Yillu8£
-50,0001=- -- -
--- -
. -30-,0_001=.-
lO,ODO/=
---S:<)()O/=
JOO,OOO!:
2S0,O()O/o:: IOO,nOD/::
30,0001=
20,(){)O/=
IO,OOO'=---
5,O(X)/=
21l0,(X)O!'-
150,000/-
---so ,oooi;;-
5_ Agr-icUltural - implements, Flour Mills,
Machme$ spares _
(a) City / MlIni<:p~ _ ~,O()O/=
(b) District GO,000/= (c) Minor settlement 20,O()O!= and ~l~ . _
uiO,O(lOr;- --
30,000/=
10,000/-'
6 . Marine spares and tools
_(~ CitY.J_~unicipa)_
------ -
2S0,(X)0/=
150,000/=-- --
l~)J2!:!..'!:J~\
_ . _ ~_ 200,(XlO/=
100,000/.:
=
No.2 Finance 2014
I
|
PRINCIPAL SUBSID1ARY CATEGORY DESCRIPTION LICENCE LICENCE
|
(e )DcEartmcntal stores
1 Cuv / Municipal |
400,OOOi=
|
300,000/=
|
||
2 District
|
200,000/=
|
200,000/=
|
|||
15
|
Endorsement
|
on
|
City, Municipal, District,
|
10,000/=
|
10,000/=
|
|
Transfer licenses
|
|
Minor settlement and villages
|
|
|
16 Duplicate license City, Municipal, District, for lost one Minor settlement and
villages 20,000/= 10,000/=
·17 lilly other business City I Mnnicieality 80,000/= 60,000/= not of national or At District headquarter 50,000/= 40,000/= international nature In Minor Settlement IS,()OO/= 15,000/=
- At village 5,000/= 5,000/=
20
-- -- -- ---------------------------
LESENI ZA VILEO ( The Intoxicating Liquors Act No.28 of 1968,Amendment No. 27-
1968,CAP 77 R.E.2002 ,Intoxicating liquors Licence fees order 1996 section(101).
Sheria ya leseni za vileo imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii:
RETAILERS ON
Leseni hii humruhusu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara
RETAILERS OFF
Leseni hii haimruhusu mtu kinywea pombe eneo la biashara bali kwa watu wanaochukua kunyewea majumbani (Take away) kama Groceries.
WHOLESALE
Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla
HOTEL
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya kunywea katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote wa mchana na usiku
RESTAURANT
Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku.
MEMBERS CLUB
Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa
Klabu na wageni wao tu.
COMBINED
Leseni ambazo zimeambatanishwa mhili kwa pamoja:
(a) Combined Hotel and retailers on
(b) Combined Hotel and Restaurant
(c) Combined restaurant and retailers on
TEMPORARY
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa kipindi kisichozidi siku tatu
LOCAL LIQUOR
Class A Local Liquor
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu ya biashara au nje ya sehemu ya biashara
Class B Local Liquor
Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya kuuza pombe za kienyeji
Class C Local Liquor
Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D au Class E
Class D Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara
Class E Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunyewea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara
1. MASHARTI YA KUPATA LESENI YA VILEO
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya
Vileo ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
2. UTARATIBU WA KUPATA LESENI
Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Manispaa au kwenye
mtandao wa Manispaa.
Eneo/jengo linalokusudiwa kufanyia biashara hiyo kukaguliwa na Afisa
Afya, Afisa Mipangomiji, Polisi, Afisa Mtendaji wa Kata (WDC) na Afisa
Biashara wa Manispaa na hutoa maoni yao kwenye fomu husika
Maombi hayo hupelekwa katika Malaka ya Utoaji wa Leseni za Vileo ya
Manispaa kwa uamuzi
• Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa Leseni baada ya
kulipa ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti.
VIWANGO VYA ADA ZA VILEO
Viwango vya ada vinavyotumika kwa sasa kwa aina mbalimbali za leseni ni kama zifuatavyo:-
1. Retailers On (Baa)
|
- 30,000.00 hadi
|
40,000.00
|
2. Retailers Off (Grosari)
|
- 20,000.00 hadi
|
30,000.00
|
3. Wholesale (Jumla)
|
- 10,000.00 hadi
|
20,000.00
|
4. Members Club (Klabu Wanachama) -
|
10,000.00 hadi
|
20,000.00
|
5. Restaurant & Retailers On
|
- 30,000.00 hadi
|
40,000.00
|
6. Temporary licence (Leseni ya muda) -
|
7,000.00 hadi
|
15,000.00
|
7. Hotel Licence (Leseni ya Hoteli)
|
- 30,000.00 hadi
|
40,000.00
|
8. Retailers Off non-spirituous
|
- 7,000.00 hadi
|
15,000.00
|
9. Retailers On – non-spirituous
|
- 10,000.00 hadi
|
15,000.00
|
Mamlaka ya Vileo itaamua kiwango cha ada kitakachotozwa kati ya kiwango cha chini na kile cha kima cha juu. Viwango vinavyotumika kwa sasa na Manispaa ni vile vya kima cha juu kwa kila aina ya leseni.
3. MASHARTI YA UTUMIAJI
Leseni za vileo zina masharti mengi ikiwa ni pamoja na kutouza kilevi
kwa watoto. Masharti mengine ni muda wa kuuza pombe,kelele za muziki na kuwa na eneo la maegesho.
MUDA WA KUUZA POMBE( Act No 27 (1) a
BAA (RETAILERS ON)
Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 Usiku
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana
na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku
GROSARI (RETAILERS OFF)
Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 2.00 asubuhi hadi saa 1.00 jioni
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 3.00 asubuhi hadi saa 6.00mchana.
RESTAURANT LICENCE (MGAHAWA)
Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana
na saa 12.00 jioni hasi saa 6.00 usiku
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00
mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00
usiku
MAKOSA
Baadhi ya makosa chini ya sheria hii:
Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanyika eneo la
biashara
Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita (16)
Kuajiri mtu chini ya miaka kumi na sita (16) kuuza pombe
Kuruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita kukaa eneo la
kuuzia pombe
Kutoweka leseni sehemu ya wazi, ambapo itaonekana kwa urahisi na
wakaguzi
Kumruhusu/kuleta fujo katika eneo la biashara
Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro
Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sheria
Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili
ADHABU
Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makosa haya akikamatwa, atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atalipa faini au kifungo au adhabu zote kwa pamoja.
UTARATIBU WA USHURU WA MALAZI (HOTEL LEVY) CHINI YA SHERIA NA. 23 YA 1972
MASHARTI YA KULIPIA HOTEL LEVY
1. Kila mmiliki wa nyumba ya wageni (Guest House) anapaswa kulipa kodi ya asilimia ishirini (20) ya malipo ya nyumba (Guest House charges) kwa mwezi husika. Wamiliki wenye mauzo yanayotozwa kodi ya zaidi ya Tshs.
40 milioni kwa mwaka hawatalipa kodi ya malazi bali watalipa Kodi ya
ongezeko la thamani (VAT) .
2. Kodi iliyowekwa, italipwa kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba ya mwezi unaofuata mauzo
UTARATIBU WA KULIPIA HOTEL LEVY
Malipo ya Ushuru wa Malazi ni lazima yaambatanishwe na fomu ya mapato ya kila siku (fomu H.L. 1) au kitabu cha wageni, na fomu ya mapato ya kila mwezi (fomu H.L.2)
Mmiliki wa nyumba analeta fomu H.L.1 au kitabu cha wageni pamoja na fomu H.L. 2 ambaye amekwisha jaza. Afisa anayekadiria atapitia H.L.1 au kitabu cha wageni na fomu H.L. 2 ili kuhakikisha ni sawa na kuhakikisha mmiliki amefikia vizuri asilimia 20 ya mapato ya malazi ya mwezi.
Mmiliki akishindwa kulipa ushuru kwa muda uliopangwa, siku saba
(7) baada ya mwezi husika kumalizika, atalipa nyongeza ya asilimia
25 ya ushuru unaotakiwa kulipwa, na endapo ataendelea kutokulipa adhabu (penalty) itakuwa inaongezeka kwa asilimia kumi (10) ya ushuru uliotakiwa kulipwa kila baada ya siku thelathini (30) kumalizika
MAKOSA
Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kushindwa kulipa ushuru wa malazi kwa muda unaotakiwa
Kushindwa au kukataa kuwasilisha fomu ya mapato ya kila mwezi
Kushindwa kuweka na kutunza kitabu chenye kumbukumbu sahihi za kulala wageni
Kushindwa kutoa risiti, hati za madai na kumbukumbu nyinginezo kama sheria inavyotaka
Kumzuia Mkurugenzi au Mwakilishi wa Mkurugenzi katika kufanya kazi
zake zilizowekwa na sheria au Kanuni za Ushuru wa Malazi
Kushindwa kutekeleza Ilani iliyotolewa na Kamishna/mkurugenzi ya kuitwa na kuwasilisha nyaraka zinazohusu nyumba yake ya kulala wageni
Kutoa taarifa ya uongo kwenye kumbukumbu yeyote inayotumika kwa ajili ya kudanganya au kushindwa au kukataa kujibu maswali vizuri kwa Afisa
wa Serikali aliyepewa madaraka na sheria hii
ADHABU
Mmiliki atakayetenda mojawapo ya makosa yaliyotajwa hapo juu atalipa faini isiyopungua Tshs. 50,000. kwa Mkrugenzi wa Manispaa na isiyozidi Laki tano (500,000) Mahakamani akipatikana na hatia.
Mmiliki anayekwepa kulipa Ushuru wa Malazi kwa makusudi akikamatwa na kutiwa hatiani atalipa faini isiyozidi shilingi milioni mbili (2,000,000.)
USIMAMIZI WA BIASHARA NDOGO NDOGO
Uendedhaji wa biashara ndogondogo unasimamiwa na sheria ndogo ya Jiji ya mwaka 1991 (The Dar es Salaam City Town/(Hawking and Street trading) amendment By – law 1999) sheria hii inalenga kuthibiti uharibifu wa Mazingira, kuhatarisha maisha/Afya za wananchi, kuleta sura mbaya ya Mji na uvamizi wa maeneo ya wazi/starehe.
MASHARTI YA KUFANYA BIASHARA
Mfanyabiashara awe safi na nadhifu
Umbo chombo safi cha kufanyia biashara
Eneo la kufanyia biashara
Kuboresha na kuhifadhi mazingira
Kuwe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria
MAKOSA
Sheria hii ndogo inamzuia mtu kufanya biashara kwenye maeneo yafuatayo:-
Bustani za Jiji /Manispaa
Mbele za nyumba za Serikali, Taasisi za Fedha, Ofisi za Ubalozi, Mashirika ya Serikali, Kimataifa, Nyumba za Ibada na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs).
Mashule, Hospitali, Maeneo yaliotengwa kwa kumbukumbu za Kitaifa.
Maeneo yanayozuia mtu kuingia na kutoka kwenye jengo.
Maeneo yenye kumzuia au kuleta usumbufu kwa watembea kwa miguu,na katika hifadhi ya barabara.
Maeneo ya kupumzikia (bus stand) au kuegesha magari.
Kutundika bidhaa kwenye majengo ya watu, Taasisi, Miti, Kuta (Fence)
nguzo za taa, Umeme, vituo vya simu, viti vya kumpumzikia wasafiri.
Kutembeza bidhaa Maofisini.
ADHABU
Mfanyabiashara atakeyetenda majawapo ya makosa haya akikamatwa atafikishwa Mahakamani na adhabu yake ni faini au kifungo au vyote kwa pamoja.
Usajili wa Taxi Cabs chini ya Sheria ndogo ya Jiji (The City of Dar es Salaam
(Registration of Taxi –cabs and Private Hire Vehicles) By-law, 1968
MASHARTI
Mmiliki wowote wa gari ndogo anayetaka kusajili gari lake ni lazima akamilishe masharti yafuatayo:
Rangi ya gari iwe nyeupe
Iwe imekaguliwa na Polisi wa Usalama barabarani na ripoti ya ukaguzi iwe imekamilika
Mmiliki awe amekwisha lipia tozo zote za Mamlaka ya Mapato na kupewa stika na leseni ya taxi (sticker and Taxi =-cabs licence) kutoka TRA Pamoja na Bima iliyo hai.
UTARATIBU
Mwombaji anatakiwa kufika na kivuli cha Kadi ya gari na awe ametimiza masharti yaliyotajwa. Atapewa fomu ya maombi ya usajili na atajaza kikamilifu na kuambatanisha:
Kivuli cha Kadi ya gari
Ripoti ya ukaguzi
Stika kutoka Mamlaka ya Mapato
Taxi – cab licence kutoka Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato
Kituo cha kuegesha
Mmiliki baada ya kukamilisha taratibu atalipa ada ya Tshs. 61,000.00 kwa
mchanganuo ufuatao:
|
Ada ya Maegesho
|
-Tshs. 36,000.00
|
|
Ada ya Usajili
|
- Tshs. 20,000.00
|
|
Ada ya Kituo
|
- Tshs. 5,000.00
|
|
JUMLA
|
- Tshs. 61,000.00
|
Baada ya malipo anapata Hati ya Usajili na namba ya ubavuni.
MAKOSA
Kufanya biashara ya taxi-cabs bila ya kusajili
Kuegesha Taxi – cab kwenye Kituo ambacho hakijaainishwa
Kutokuwa na ripoti ya ukaguzi ya Polisi wa Usalama barabarani
Kutokuwa na Leseni ya Taxi-cab
Kutokuwa na Stika
ADHABU
Anayefanya kosa lolote atakamatwa na Mamlaka inayohusika na kufilishwa kwa kosa hilo.
12
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.