Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mheshimiwa Simon Simalenga ameitaka Halmashauri ya Mji Bariadi kuongeza umakini kwenye ukusanyaji wa mapato huku kukiwepo na mikakati thabiti ya namna bora ya ukusanyaji mapato.
Mheshimiwa Simalenga ameagiza Halmashauri ya Mji Bariadi kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari ili kurahisisha shughuli ya ukusanyaji mapato huku akitaka bajeti iendane na mahitaji ya wananchi.
Aidha ameagiza kuweka udhibiti na kuongeza umakini kwenye zao la pamba na mbegu za pamba kwa kutaka uwepo na ushirikiano ili kudhibiti ubadhilifu wowote unaoweza jitokeza.
Ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupitisha Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 katika Halmashauri ya Mji Bariadi
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mji Bariadi
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.