Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Bariadi ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Imelda Kirima amewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ya Tshs 29,235,121,948.00 ambapo amesema mapendekezo hayo yamefanyika kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria ya Bajeti,Sura Namba 439 na kanuni zake za Mwaka 2015.
Aidha ameongeza kuwa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali uliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango Mwaka 2025/2026,Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Pia Mpango Mkakati wa Halmashauri ya Mji Bariadi (2021/22-2025/2026),Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2021/22-2025/2026) na agenda ya Afrika Mashariki 2050 ya Dira ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika 2050.
MWISHO
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.