Afisa Habari - Halmashauri ya Mji
Serikali ilileta kiasi cha Shillingi Millioni 250 kwa ajii ya ujenzi na uanzishwaji wa shule mpya ya msingi ambayo itaenda kuondoa pamoja na kupunguza tatizo la msongamano wa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni hali ambayo inaweza sababisha ufaulu wa wanafunzi kushuka.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ilileta fedha hizo kiasi cha Shillingi Million 250 kwa ajii ya ujenzi na uanzishwaji wa shule hiyo ambapo mpaka sasa shule hiyo ina jumla ya vyumba vya madarasa 9,matundu ya vyoo 30 pamoja na jengo la utawala huku kukiwa na wanafunzi 543 kuanzia awali hadi darasa la tatu pamoja na walimu 5.
#Halmashauri ya Mji Bariadi
#Bariadi
#Simiyu
#kaziiendelee
Along Bariadi-Lamadi Road
Anuani ya Posta: P. O. Box 526, Bariadi
Simu ya Mezani: +255 (28) 2700554
Simu: ******
Barua Pepe: info@bariaditc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.